MGOMBEA
anayeomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Steven Wasira, amesema hana majina ya
washukiwa wa ufisadi, ingawa uovu huo umo ndani ya vyama vya siasa
ikiwamo CCM.
Wasira
anayeongozwa na kauli mbiu ya Uadilifu na Umoja wa Watanzania; Safari ya
Uhakika, alisema hayo wakati akizungumza na wana-CCM waliomdhamini
katika mikoa ya Rukwa na Katavi jana.
Alisema
CCM na serikali yake ni taasisi zilizo na misingi ya uadilifu, ingawa
ndani yake kuna uwezekano wa kuwapo watu wanaotuhumiwa kwa uhalifu huo.
Alisema
ufisadi na rushwa na miongoni mwa matatizo makubwa yanayoiathiri jamii
na kwamba taifa linamhitaji kiongozi asiyekuwa na kashfa inayomfanya
atiliwe shaka katika kukabiliana na kadhia hiyo.
“Hapa
sina majina ya mafisadi lakini ninaamini kwamba si ndani ya CCM pekee,
bali hata katika vyama vingine vya siasa, rushwa na ufisadi ni miongoni
ma matatizo makubwa yanayovikabili,” alisema.
Wasira
alisema kutokana na hali hiyo, vita dhidi ya rushwa na ufisadi inapaswa
kuwa katika misingi ya hoja na uthubutu wa kuidhibiti badala ya kumlenga
mtu binafsi.
Alisema
Tanzania ina taasisi imara ambazo zikitumika ipasavyo zitachochea
kuwatambua washukiwa wa ufisadi, vitendo vinavyoashiria uhalifu huo na
kuchukua hatua kwa ukali na haraka.
Wasira
alisema ikiwa CCM itamteua kuwania na hatimaye kuwania Urais, imani yake
ni katika kutoa uhuru na mamlaka zaidi kwa vyombo husika vikiwamo vya
sheria, kutekeleza majukumu bila kuoneana aibu.
Alisema,
“ninapozungumzia ufisadi sizungumzii mtu au watu, tunauzungumza ufisadi
kama hoja, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hata ndani ya CCM kuna
viashiria vya ufisadi, lakini haimaanishi kwamba CCM ni chama cha
kifisadi.”
Aliongeza,
“hata kwa upinzani kuna ufisadi pia, hivyo ufisadi ni tatizo kubwa
katika jamii yetu, kama nitapata fursa ya kuliongoza Taifa letu
nitahakikisha tunaukabili kwa nguvu zote ili kurejesha heshima na hadhi
ya nchi yetu,” alisema.
Alisisitiza
umuhimu wa kupiga hatua katika kilimo na viwanda ikiwa ni moja ya njia
kuu za kukuza uchumi na kuboresha maisha na ustawi wa wananchi. (DK)
Kwa
mujibu wa Wasira, kilimo pekee ndicho kinaweza kuzalisha ajira nyingi
kwa vijana kuliko sekta nyingine pamoja na kuliingizia Taifa pato kubwa
zikiwamo fedha za kigeni.
Wasira
alizungumzia ajira kwa vijana na kusema hivi sasa kuna kasi ya vijana
wengi kukimbia kutoka vijijini kutokana na umasikini unaowakabili, na
kwenda kukutana na umasikini mwingine mijini.
Alisema
uboreshaji wa kilimo, uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya kuongeza
thamani za mazao kutatoa hamasa kwa vijana kushiriki kilimo na
kutengeneza ajira.
Leo
Wasira anatarajiwa kuwasili mkoani Kigoma kutafuta wadhamini, ukiwa ni
mkoa wa 30 tangu aanze safari ya kutafuta wadhamini Juni 3, mwaka huu
ambapo alianzia mkoani Dodoma.
Vikao vya
uteuzi vinatarajiwa kuanza mjini Dodoma Julai 5, mwaka huu, ambapo
mgombea urais kwa tiketi anatarajiwa kupatikana Julai 11, na Uchaguzi
Mkuu umepangwa kufanyika mwezi Oktoba.
0 comments:
Post a Comment